house girl

Waigizaji:- Mama Lutha,Baba Lutha,Mamtei,Lutha
Maranyingi wafanyakazi wa ndani wametuhumiwa kwa mambo mbalimbali hasa wizi na kuteka nyumba za watu kwa hisia za mapenzi.
Sijui nani alaumiwe kati ya mume ,mke au msichana wa kazi...Filamu inaenda hivi baada ya mamaRuta kumfuata msichana kijijini kwao nakumleta mjini mumewe anamtamani na kufanikiwa kumshawishi kimapenzi ndipo watoto wake wanatambua na kumwambia mama yao pamoja na kumpa kichapo housi girl...kwa uhondo zaidi isake uje uchangie umeionaje??
Revenge

Muongozaji:-Vicent Kigosi 'Ray'
waigizaji:-Johari, Ray,Magari,Mainda, Tea
Ni filamu inayoonyesha kisasi kama ilivyo jina lake, ambapo Ray anasafiri kikazi na rafikie bila baraka za mkewe ambaye alikuwa ni mja mzito akiwa masomoni anapewa taarifa mkewe ni mgonjwa anaamua kurudi na kukuta mkewe Tea kafariki na kujikuta anakosa yote kazi na mke...ndipo anakutana na Johari akiwa na mtoto mdogo baada ya kufukuzwa na wazazi baada ya kupewa mimba na mzazi mwenzio kumtelekeza, wakaamua kuishi pamoja ndipo rafikie Ray anarudi kutoka masomoni nakuja kumuangalia Ray na kukutana na Johari mwanamke aliyempa mimba ndipo kisasi kilipoanzia na mauaji yanafanyika
She is my sister

Waigizaji:Kanumba, Monalisa, Nkiru Sylvanus (Nigeria)Mercy Johnson (Nig)
Mtayarishaji Mtitu Game na Ogedegbe Film(Nig)
Ni filamu inayohusu mahusiano kwa ujumla ambapo Kanumba anaopokelewa na Monalisa akiwa choka mbaya kijijini na kuja mjini anapigwa soap soap na kupendeza anatekwa na penzi la shoga ake Monalisa Nkiru. na kuamua kummwaga Monalisa na kumtelekeza na mtoto na kumnyang'anya malizake
Mdogo wake Mona anafunga shule kuja mtembelea dada yake anakutakana na hicho kisanga na kuamua kulipiza kisasi kwa kumlaghai kanumba na kufanikiwa kumteka kimapenzi na kurejesha vitu vya dada yake vyote na kuamuacha kanumba mtupu......na hapo ndo Mohalisa alisikika akisema..... She is My Sister ..My Savior